Big Jah Man Kuhusu Albamu Yake, Kifo Cha Steve 2K Na Utamaduni Wa BongoFlevaMwanamuziki Big JahMan amevunja ukimya na kuweka wazi kile kinachotajwa kutokua na Albamu mpaka sasa licha ya kuwepo kwenye game ya Bongoflava kwa muda mrefu. Akipiga stori na SEETHEAFRICAN TV Big JahMan amesema ishu ya kifo cha mwanamuziki wa zamani Marehemu Steve 2K ni moja ya tukio ambalo hawezi kusahau kwani licha ya kumkosa mshikaji wake (Steve 2k) hata mipango yake mingi ilisimama kutokana na mazingira ya kifo kumuhusisha producer aliekuwa akifanya nae kazi hivyo hata maandalizi ya Albamu yake hayakuendelea tena mpka alipoamua kujipanga upya. Kwenye sentensi nyingine Big Jah Man amewataka wanamuziki wa Bongo kuupa heshima muziki wetu kwa kufuata misingi Bongoflava na utamaduni wa Kiafrika.

MTAZAME HAPA:


Kwa sasa Big Jah Man anatamba na ngoma yake Mabundi chini ya usimamizi wa Label "Cheusi Dawa" ya rapa FidQ.

MABUNDI - Big Jahman Ft Fid Q, SaRaha (Official Video)

No comments