Good News Kutoka Kwa Kendrick Lamar Na RihannaApril 14 mwaka huu rapa Kendrick Lamar aliiachia album  "Damn" ambayo imefanikiwa kufanya poa na kwani ngoma zote 14 zilitisha kwenye chati za Billboard Hot 100. Ngoma kama Humble ambayo ilitoka mwezi mmoja kabla ya kuachiwa kwa Albamu hiyo imeendelea kuwa wimbo pendwa zaidi ikifuatiwa na DNA ambayo ndani ya mwezi mmoja sasa video yake imejikusanyia views zaidi ya milioni 99 kwenye chaneli yake ya Vevo.

Nyingine ambayo inaendelea kufanya poa ni"Loyalty" ambayo BadgirlRiRi (Rihanna) amepewa shavu, Video inayoonekana mitandaoni inatosha kutuambia kuwa kinachoendelea sasa hivi ni utengenezwaji wa video ya ngoma hiyo.

  ''Namkubali sana Rihanna Mara nyingi nimekua nikifikiria kufanya nae kazi ni mwanamke anaeongea kwa niaba ya wanawake wengi, Rihanna amekua mfano wa kuigwa na wasichana wengi kupitia harakazi zake za kimuziki, Niliandika ngoma na haraka mno nilimfikiria yeye, Nilifanikiwa kumuingiza studio na mzigo ukawa umekamilika". Alisema Kendrick Lamar kwenye moja ya Interview alipoulizwa kuhusu kumshirikisha Rihanna.

Wakati hayo yakiendelea Rihanna ametajwa kufanya ngoma na Bryson Tiller ambayo itapatikana kwenye Albamu ya DjKhaled "Greatful" 
Theme images by rami_ba. Powered by Blogger.