FullData Kuhusu Hassan Jameel Bebe Mpya Wa Rihanna

Kuanzia jana kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii zilienea picha za Badgirl RiRi akiwa kwenye mikao ya kimahaba na mwanaume ambae hakujulikana mara moja.


 Huku na huku mapaparazi kufuatilia unaambiwa mshikaji anatokea kwenye moja kati ya familia kubwa ambazo ziko vizuri. 
Hassan Jameel ndilo jina lake ni raia wa Saudi anatajwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya familia yao, Abdul Latif, moja kati ya makampuni yanayotajwa sana kwenye headlines za biashara duniani. Familia yake pia inamiliki Hisa kwenye kampuni ya TOYOTA na wanatajwa kuwa na utajiri wa dola za kimarekani bilioni 1.5 (sawa na bilioni 34.8 za Kitanzania)

Rihanna na babe wake huyo mpya wapo nchini Hispania wakijiachia kwa raha zao huku wakijaribu kwenda mbali na upepo wa mapaparazi ambao tayari wameshafanikisha moja ya majukumu yao. 
 


 Kikichimba ndani zaidi chanzo cha stori hiyo kimeiambia DailyTimes kuwa Jameel anatakiwa ale vyake asepe maana hawezi kuwa peke yake kwenye macho ya Rihanna ambae kwa muda sasa amekua hayupo kwenye mahusiano ya kueleweka,