Tamasha La Vunja Bei Expo Laacha Historia Dar Es SalaamTamasha la #VunjaBeiExpo lililofanyika Juni 2-4 kwenye viwanja vya Posta (Sayansi) Kijitonyama laacha historia bada ya wakazi wa Jiji la Dar es salaam kujipatia bidhaa mbalimbali kwa bei sawa na bure, Kama jina la Tamsha lilivyo unaambiwa kila kitu kiliuzwa kwa bei iliyovunjwa. 
Tamasha La #VunjaBeiExpo lilikusudiwa kuwa la aina yake kwa kuwasogeza wauzaji wa bidhaa mbalimbali na wanunuzi wao sehemu moja. Vunja Bei Expo ilihusisha Makampuni, Wafanyabishara na wajasiriamali wadogo wadogo. Kwa muda wa siku tatu wakazi wa jiji la Dar es salaam walinufaika kwa kujipatia bidhaa mbalimbali kama simu, nguo, vyakula, vinywaji, vipodozi, vyombo vya ndani, bidhaa za wajasiliamali, nk.  
Taasisi mbalimbali zilifikisha bidhaa zao viwanjani hapo kwa zoezi la uvunjaji bei tu. Miongoni mwa taasisi hizo ni Vodcom Tanzania, Ttcl, Windhoek, Sayona Drinks Limited, KukuPoa, Udzungwa drinking water, Temnar Company Limited, na nyingine nying pamoja wafanyabiashara wadogo. Tamasha lilipambwa na nyama choma, michezo ya watoto na michezo ya promotion ambapo zawadi kutoka kwa makampuni shiriki zilitolewa. 
Vunja Bei Expo ilipewa nguvu na Vodacom Tanzania, TTCL, Sayona Drinks Limited, Udzugwa drinking water, Dream fantasy na Times FM.   

KUHUSU VUNJA BEI EXPO: 

Vunja Bei Expo ni tamasha linaloandaliwa makhususi kwa ajili ya kutoa fursa kwa wafanyabishara kuuza bidhaa zao mbalimbali kwa wingi na kuwapa watu nafasi ya kujipatia mahitaji yao mbalimbali kwa bei nafuu. Baada ya tamasha hili kuzinduliwa tarehe 2 -4 Juni 2017 imetangazwa kuwa Tamasha hili litaebdelea kufanyika sehemu mbalimbali za Jiji la Dar es salaam pia sehemu nyingine mbalimbali nchini kuanzia mwishoni wa mwezi Julai 2017.

No comments