Alichokisema @DJKhaled Kuhusu Traviss Scott Na Grateful


DJ Khaled yupo mbioni kabisa kudondosha "Grateful" Project ambayo inaweza kuwakusanya wanamuziki zaidi ya kumi wenye majina makubwa na kuwakutanisha pamoja.

Mwishoni mwa mwezi April Justin Bieber, Quavo, LilWayne na Chance The Raper walikutana kwenye ngoma "I'm The One" ambayo ilifanikiwa kuwa ngoma kubwa ndani ya muda mfupi,

 
Ikiwa bado haijamalizika ladha ya utamu wake, juzi jumatatu DJ Khaled ameitambulisha "To The Max" na Drake huku picha ya mtoto wake Ashad ikitangazwa kama official ArtWork ya Album "Grateful" 

 
Sambamba na utambulisho wa Artwork na wimbo mpya na Drake, Dj Khaled aliahidi kuiachia ile tracklist ya "Grateful" Ijumaa ya wiki hii lakini kabla ya kuzianika ngoma zote akataka mashabiki wafahamu kuhusu Traviss Scott amepata shavu kwenye ngoma 4 ndani ya Grateful itakayoingizwa sokoni June 23. 

No comments