Fahamu Kilichopelekea Bifu Ya Baraka The Prince Kwa Ben Pol Na Jux


Baraka the Prince anatajwa kuingia kwenye bifu kubwa na wanamuziki wenzake Ben Pol na Jux. Ben Pol ameeleza chanzo cha kilochosababisha wao kutoelewana ingawa walikua washikaji. Ben Pol na Baraka wamewai kushirikiana kuachia wimbo unaoitwa ‘Mwambie’. Hata hivyo wiki mbili zilizopita Baraka alimkashifu Ben Pol alipowachia wimbo wake mpya ‘Tatu’.

 Ben Pol amefunguka kilichotokea kati yake na Baraka the Prince; kwenye mahojiano na Ayo TV, Ben Pol alisema Baraka alianza kuwa na chuki na yeye na Jux baada ya wao kumpuguza kimuziki kwa kushirikiana kufanya shows pamoja na tours
 “Mimi napenda sana kukoselewa, napenda kupokea maoni lakini ina matter sana maoni yanatoka kwa mtu gani au wewe na huyu mtu mko kwenye situation gani.
Baraka maoni yake yanaweza yakawa mazuri, yanaweza yakawa ni ya kuboresha, yanaweza yakawa ya kujenga, kukosoa. Lakini mimi nawaza status yangu na Baraka ilivyo halafu nahusianisha na yale maoni yake, naona kuna msuguano.

Baraka anatuchukia mimi na Jux, Hata last time tulikutana naye alikua hataki kutusalamia akageuza mgongo kabisa…muda mrefu kama wiki tatu…Hataki kutusalamia ameweka mgongo hivi. Tumeenda kumsalamia Baraka, ‘Baraka tumekuona, umependeza na tumekumiss’, lakini alikua hataki kuongea na sisi, alikua na chuki. “Sasa mtu ambaye ana chuki, ana tatizo na wewe akitoa maoni kuhusu kitu chako unakua na mashaka kidogo kwamba ni honest opinion au kwasababu ya misunderstanding ambayo mnayo.

Na Baraka hii source ya kutuchukia mimi na Jux sababu tulimpunguza kwenye umoja ambayo tulikua tumeuanzisha kufanya shows, kufanya tours…tulimpunguza. Hatukuwai kusema, hatukuwai kumuaibisha kwenye media kusema kwamba tumempunguza au nini… Ni mdogo wetu tumesema tumlindie heshima, tumempunguza lakini hatutasema hivyo kwenye redio au kwenye mtandao…kwenye sehemu yoyote. Lakini kumbe yeye alikua na kinyongo, kwanzia hapo ukimtumia post, ukimwambia kitu akusaidie kushare anakuwekea hivi ‘hapana, no’, si support’. Kwa hivyo tunasema kwamba ana chuki. Na kumpunguza ilikua lazima tumpunguze kwasababu ya discipline, kukosa nidhamu. Ilikua lazima tumpunguze.” Ben Pol alisema.

ANGALIA HII VIDEO YA AYO TV HAPA:

No comments

Theme images by rami_ba. Powered by Blogger.