Mungu Ni Wetu Sote @SnoopDogg Atakuthibitishia Hapa


Mungu ni wetu sote, Unaweza kuwa ni msemo maarufu sana masikioni mwako lakini kwa mawazo ya binadamu wa kawaida  sio rahisi tu kusema "Mungu Ni Wetu Sote" halafu akamaanisha, Either ukubali or ukatae Snoop Dogg yupo tayari kuishangaza Dunia kupitia msemo huo.
Kwa mujibu wa video kwenye ukurasa wake wa Instagram Baba'ko anaonekana akiwa studio akiimba wimbo wa dini tena kwa hisia kali, Ishara tosha kutuambia kwa Mungu hakuna mbishi.
 

Kumbe hajaishia kuonyesha hisia zake bure. Vyanzo vya karibu yake vimedai Snoop amekua busy akitengeneza Albamu yake itakayokuwa na nyimbo za dini tu. 

Tumemzoea jamaa kwenye muonekana wa kihuni na ngoma zake za kufoka, Unafikiri kwenye Gospel atatisha?

No comments