Nyumba Ya Milioni 894 Ambayo Beyonce Na JAY-Z Wamepanga Kwa Ajili Ya Mapacha Wao.


Beyonce na JAY-Z wameripotiwa kuwatoa watoto wao mapAcha hospitali walikozaliwa mapema mwezi huu na kuwapeleka nyumbani, Kwa mujibu wa TMZ couple hiyo inadaiwa kupanga mjengo wenye vyumba kumi vya kulala na eneo kubwa linalowatosha kujiachia bila kubugudhiwa kivyovyote vile unaolipwa dola 400,000 (Sawa na  894,800,000/= za kitanzania) kwa mwezi.

Chanzo cha karibu na fmilia hiyo kimeiambia TMZ kuwa familia nzima ya The Carter yaani Jay, Beyonce na watoto wao watatu watahamia kwenye nyumba hiyo mpya mpaka watakapopata nyumba ya kudumu pande za Los Angels,

Sio tu mapacha ambao Beyonce atajivunia kuwapata mwezi huu ushindi wa vipengele 7 ikiwemo Msanii Bora wa Kike na Album Bora (Lemonade) kwenye Tuzo za BET zilizofanyika Wikiendi iliyopita ni kitu kingine Beyonce anajivunia.

Theme images by rami_ba. Powered by Blogger.