Zawadi Ya Saida Karoli Kwa @VictorWanyama

Staa wa Soka Mkenya Victor Wanyama alitembelea Tanzania takribani wiki Moja iliyopita kwasababu ya mapumziko, kiungo huyo wa Tottenham Hotspur pia alihudhuria mashindano ya soka alipokua nchini.

Serikali ya wilaya ya Ubungo ilimpa heshima Victor Wanyama kwa kuipa moja ya barabara za Ubongo jina la nyota huyo ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa Ndondo Cup 2017 kati ya FC Kauzu dhidi ya Faru Jeuri.

Hata hivyo serikali hio ilibadilisha hatua ya kuipa moja ya barabara jina la Wanyama wakidai kuwa utaratibu haukuzingatiwa

Licha ya kuzuiwa kutumika jina Lake kwenye Moja ya mitaa Ya Ubungo, staa huyo wa Tottenham alipata zawadi nzuri kutoka wa Saida Karoli.

Victor Wanyama na Saida Karoli walikutana kwenye studio za Clouds FM ndipo Wanyama alipofunguka kuwa yeye ni Fan mkubwa wa Saida Karoli.

Na kwa bahati nzuri siku waliyokutana ilikua birthday ya Wanyama ambaye alikua anatimiza umri wa miaka 26; Saida Karoli alimpa Wanyama CDs zake kama zawadi.

“Thank you @saidakarolitz for the CDs,I’m humbled,” Wanyama aliandika kwenye kurasa
Zake za Mitandao ya kijamii.

No comments

Theme images by rami_ba. Powered by Blogger.