21 Savage Kawachana Wanaobeza Mapenzi Yake Na Amber Rose, Hayupo Kama Wanavyomfikiria


Shayaa Bin Abraham-Joseph maarufu kama 21 Savage rapa mamrekani anaewakilisha kitaa cha Atlanta, Georgia (Moja kati ya majiji yenye rappers wengi). Mshikaji ni chalii mwenye miaka 25 tu ambae amekua akitajwa kuzama kwenye mahusiano ya kimapenzi na babymama wa Rapa Wiz Khalifa, Amber Rose mwenye umri wa miaka 34.

Kwenye moja ya interview alizofanya, 21 Savage amethibitisha tetesi hizo kwa kuweka wazi mahusiano yake na Amber Rose ambayo yamekua #TalkOfTheTown..

"....ni mwanamke wa kipekee, amekua akinishawishi kufanya makubwa zaidi ambayo sikuwahi kufikiria kufanya, ananikumbusha vitu vya msingi... " amesema 21 Savage.

 Siku za hivi karibuni rapa 21 Savage ametajwa kwenye headlines za mitandao na Media mbalimbali kwa kujihusisha na Amber Rose anaonekana Kumzidi umri kwa zaidi ya miaka 9 huku wengine wakienda mbali zaidi na kusdai mshikaji anafundishwa maisha ya ustaa..

Kwenye kauli nyingine rapa huyo anaeshine na Albam #ISSA amewataka wanaoibeza couple yake kukaa mbali na biashara hiyo kwani hakuna inaemuhusu zaidi ya Mungu.