Ujanja Ujanja Wamtokea Puani Rappa DMX


Rappa wa siku nyingi mkongwe DMX amekamatwa Alhamisi ya jana, Kwa mujibu wa mtandao wa  THR, mamlaka ya Mapato kipande cha New York imemkamata  kwa madai rappa huyo anajaribu kukwepa kodi ambayo inatajwa kuwa dola milioni 1.7.

Ripoti ya wakili wa serikali imesema DMX alikwepa kodi kwa kufungua akaunti yenye jina tofauti kisha kuingiza mkwanja wake. Madai hayo yameongeza kuwa rapa huyo alikataa pia chek ya malipo aliyopewa na mtandao wa VH1 kwa madai asingeweza kuipokea mpaka kiondolewe kipengele cha malipo ya Kodi.

Imekuwa ni mara kadhaa sasa kwa rappa huyo kuwa na matukio yanayofanana na hayo mpaka serikali ya mji wa New York kuamua kumweka chini ya ulinzi mpaka Jumatatu atakapofikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.