New Music Ommy Dimpoz - Cheche


Baada ya mafanikio ya kutosha kwenye hitsong "Kajiandae" Ft. AliKiba, Miezi sita baadae Ommy Dimpoz amerudi na "Cheche",

Wakati akitambulisha wimbo huo kwenye "XXL" ya Clouds FM Ommy Dimpoz amesema ni wimbo ambao aliandikiwa na Producers Kidboy na LolPop, Kwenye sentesi nyingine Ommy Dimpoz amekaririwa akisema kuwa "Cheche ni wimbo ambao ameukubali na kuamua kuuachia muda huu kwa sababu anaamini ni aina ya muziki ambao utaishi.

Alikiba ambae alimsindikiza mshikaji wake huyo amesema tangu siku ya kwanza alipousikia wimbo huo aliukubali na hata kufanya aanze kuimba na ilifika pointi hata alisahau wimbo huo aliusikia wapi"

Cheche inakuja sambamba na kutangazwa kwa Ommy Dimpoz kama mwanamuziki mpya anaeungana na Alikiba, JideJayDee na Baraka Da Prince chini ya usimamizi wa kampuni ya "ROCKSTAR4000"


DOWNLOAD "Ommy Dimpoz - Cheche"


 

Confirmed! @OmmyDimpoz Amelamba Deal Na Management Kubwa Afrika...: