Spotify Yakanusha Kutengeneza "Fake Artist" Kwa Ajili Ya Kupiga Mkwanja Mrefu
Uongozi wa mtandao wa spotify unaotoa huduma ya ku-stream muziki umetoa tamko kuhusu ripoti iliyoandikwa na mtandao wa Vulture kuhusu tetesi za kuwa na wasanii feki (Wasiokuwa na vigezo vya muziki)  kwa ajili tu ya kuingiza mkwanja kupitia playlist za ngoma zao ambazo zimekua hazidumu kwenye game kutokana na kutokidhi viwango vya ngoma kali.

 "Hatuna na wala hatujawahi kutengeneza wanamuziki "Feki", Kauli ya Vulture ni uongo mtupu...  Spotify  sio label, kazi yetu ni kukusanya ngoma kutoka kwa wahisani na kuziingiza kwenye mfumo wetu halafu watu wanaamua wasikilize nini, hicho ndicho tunachofanya, ishu ya kutengeneza "Fake Artist" sio kweli  hiyo ni sawa na kujilipa pesa yetu wenyewe, hatuwezi kufanya hivyo ili tupige mkwanja mrefu ni uongo ipuuzwe.. Msemaji wa kampuni hiyo ameiambia Billboard..

Ripoti iliyoandikwa kwenye Jarida la Volture inautuhumu Spotify kutengeneza wasanii wasiokuwa na uwezo mkubwa wa muziki kwa ajili ya kuwa na idadi ya ngoma nyingi kwenye mzunguko lakini ni ngoma ambazo zimekua hazid