Alichokisema Diamond Platnumz Kuhusu HeadPhone Za "Chibu Beats" Na Dr. Dre
Baada ya ukimya wa muda mrefu tangu msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz atangaze ujio wa bidhaa zake za headphone ‘Chibu Beats’, msanii huyo amefungukia sababu za kuchelewa kudropishwa kwa mzigo huo.


Kwa mujibu wa Bongo5 muimbaji huyo ameiambia XXL ya Clouds FM kuwa bidhaa hizo zimechelewa kutokana na mchakato wa usajili wa jina.“Katika usajili wa Chibu Beats jina lilileta matatizo kidogo, ilikwamisha hapo kwa sababu neno beats mtu kashalisajili dunia nzima mtu mwingine asilitumie neno la beats, siunajua ni la Dre. Kwa hiyo tunaweka namna nyingine ambayo itakuwa nzuri, zitatoka zimeshakuwa tayari mpaka sampo, tumeshasikiliza ni fresh sound hatari” amesema Diamond.
Theme images by rami_ba. Powered by Blogger.