Baada Ya Tatu Ben Pol Kuwakutanisha Stamina Na Roma Mkatoliki

Msanii Ben Pol ambaye sasa anafanya poa na wimbo wake 'Tatu' amefunguka na kusema watu wajiandae kwani kuna ujio mkubwa wa wimbo wa wasanii wakubwa watatu akiwepo yeye mwenyewe, Roma Mkatoliki na Stamina.
  
"Nilikuwa na (Studio Session) na  Roma Mkatoliki, Stamina na Manecky, hicho kitu kilichofanyika hapo ni hatari sana, yaani ni 'Fire' naomba watu wajiandae tu kwa hilo goma" Benpol aliiambia FNL ya EATV

Ben Pol amedai wimbo huo ambao umeweza kuwakutanisha pamoja yeye, Roma Mkatoliki pamoja na Stamina ni wimbo wa pamoja wa kushirikiana.

No comments

Theme images by rami_ba. Powered by Blogger.