Huenda TheWeeknd Akaliamsha Dude Huku #StarBoyTour IkiendeleaKwa mashabiki na wapenzi wa muziki wa Starboy The Weeknd ambao mmeshanza ku-miss ladha ya staa wenu huenda muda si mrefu kiu yenu ikakatwa na burudani ya ngoma kali kutoka kwa mkali wa ngoma ya "I Feel It Comming"

Kupitia ukurasa wake wa Instagram The Weeknd ametupia picha inayomuonyesha akiwa kwenye chumba cha kurekodia huku caption ikiwa ni "Making Noises", Hakuna ambae amepata chance ya kusikia ambacho The Weeknd anafanya, Labda watu wake wa karibu. Tunachojaribu kufikiria labda jamaa anajiweka busy zaidi ili ujio wake uwe mkali zaidi ya ule wa albamu yake "Starboy".


A post shared by The Weeknd (@theweeknd) on

The Weeknd yupo kwenye ziara ya #StarboyTour ambayo kwa kipindi hiki cha mwezi Julai atakua anazunguka Bara la Ulaya halafu akimalizia na North America mwezi Agosti mpaka Septemba.
Theme images by rami_ba. Powered by Blogger.