Instagram Yasababishia Shilole Kushindwa Kuachia Wimbo Mpya, Kuolewa Je?


Zuena Mohamed, Maarufu kama Shilole Kiuno, Shishibaby au Shishi Trump Jumatano, Julai 26 amepiga stori na 5Selekt ya EATV na kufungukia ishu kibao kuhusu maisha yake binafsi na muziki wake,

Miongoni mwa vitu ambavyo Shilole ameweka wazi ni kuhusu mahusiano yake ya kimapenzi, "Sina boyfriend, nina mchumba kabisa na tayari ameshatoa barua kwahiyo muda wowote tunaweza kufunga ndoa" alisema Shishi.

Kwenye sentensi nyingine Shilole amethibitisha kama mahusiano ya mashoga zake na wanaume wake wa zamani hayamnyimi usingizi hata kidogo "Ninachoamini mapenzi ni kama Daladala, Ukishuka wenzako wanapanda so acha wajiachie, mimi sina tatizo kabisa" Aliongeza Shilole

Shilole ambae kwa mara ya mwisho aliachia remix ya wimbo wake "Hatutoi Kiki" aliyomshirikisha Mnaijeria Waje amesema anatamani kuachia ngoma mpya lakini kitendo cha wahuni wa mjini kui-hack Instagram akaunti yake kumemfanya arudi nyuma hatua nyingi zaidi mbali sana na mashabiki wake.

"Natamani kuachia ngoma mpya lakini nashindwa maana niko mbali sana na mashabiki zangu baada ya Instagram page yangu kuibiwa nimerudishwa nyuma hatua nyingi" Alimaliza Shishi


ANGALIA BALAA LA SHILOLE NA ADM MCHOMVU KWENYE HII VIDEO:
 

No comments

Theme images by rami_ba. Powered by Blogger.