Japan Yamponza Justin Bieber, Haruhusiwi Tena Kuingia China

Staa wa muziki wa Pop kutoka Canada Justin Bieber amepigwa marufuku kuingia nchini China.

Kwa mujibu wa Wizara ya Habari nchini humo ni marufuku kwa wanamuziki/watu maarufu ambao wamejihusisha katika vitendo vya "utovu wa nidhamu" kuruhusiwa kuingia nchini humo.

"Justin Bieber ni mwimbaji mwenye kipaji, lakini pia ni mwanamuziki kijana mzuri,"msemaji wa wizara hiyo alisema alipokua akijibu swali la shabiki aliyetaka kujua kwanini ratiba ya Bieber haionyeshi mji wowote wa China licha ya staa huyo kuwa na ziara ya kimuziki kwenye bara la ASIA.

"Tunatumaini Justin Bieber atakapokomaa, anaweza kuendelea kuimarisha maneno yake na matendo, na kuwa mwanamuziki anayependwa" aliongeza.

Ishu hiyo inakuja baada ya Bieber  kupost picha aliyopigwa akitembelea madhabahu ya Yasukuni jijini Tokyo, Japan

Madhabahu hayo nchini Japan yalijengwa kwa heshima ya wanajeshi waliouawa vitani pamoja na wahalifu wa kivita lakini nchini China na Korea Kusini, hutazamwa kama ishara kwamba Japan haijajutia makosa yaliyotendwa na watawala wa nchi hiyo China na Japan miaka ya nyuma.

 Mara ya mwisho Bieber alitembelea China mwaka 2013, lakini sasa amejiunga na orodha ndefu ya wanamuziki waliopigwa marufuku kufika nchini humo.

Wengine ni bendi ya  Oasis ya Oasis na kundi la  Maroon 5.

No comments

Theme images by rami_ba. Powered by Blogger.