Justin Bieber Katajwa Kwenye Ajali Ya Barabarani Siku Ya Julai 26Kuna Video Clip  inayoonyesha gari la muimbaji Justin Bieber likimgonga mtu aliekuwa akitembea kwa miguu baada ya kutoka katika ibada ndani ya kanisa moja mjini Los Angeles siku ya Jumatano

Idara ya polisi mjini Beverly Hills imesema kuwa gari hilo lilikuwa likiendeshwa kwa mwendo wa polepole wakati wa ajali hiyo.

Maafisa wa polisi wa eneo la Beverly Hills waliwasili katika eneo la ajali hiyo na kumkuta mwanamume mmoja ambaye alikuwa amelala chini ambae baadae alipelekwa hadi hospitali licha ya kutokua na majeraha ya kutisha.

Bieber alibaki katika eneo hilo la ajali kushirikiana na maafisa wa polisi na baadaye akaachiliwa.
Bieber alionekana amesimama na kuzungumza na mtu aliyejeruhiwa ambaye alitambuliwa kuwa ni mpiga picha.

Sajenti Stout alithibitisha kwamba Bieber alitoka nje ya gari lake na kujaribu kumpatia huduma ya kwanza baada ya ajali hiyo.

No comments

Theme images by rami_ba. Powered by Blogger.