#Video | Kanye West Na Migos Studio Moja, Fujo Mpaka Usiku Mnene...Imekua ni kawaida sasa kwa rapa Kanye West kuonekana akikatiza mitaa tofauti na wakati wa nyuma alipokua akijaribu kukwepa kuonekana ovyo kwenye media, 

Kitu kinachoonekana kushangaza na kuwafanya mashabiki wa Kanye kuwa makini zaidi kwa kusubiri kinachoweza kutokea ni video wanayoonekana Quavo, TakeOff na OffSet wanaounda kundi la Migos wakiingia kwenye studio ambayo mnyamwezi Kanye alikua pande hizo mpaka usiku mnene.


Sio mabosi wa DefJam Music peke yao tu, hata Kanye nae amekua akikwepa swali kuhusu  tetesi za ujio wa Albam mpya mwaka huu,
 Huenda hii ya Migos ikawa ndio ishara ya kuthibitisha hilo.

Theme images by rami_ba. Powered by Blogger.