Rais Wa Manzese @MadeeSeneda Kwa Hili Amezingua

Takribani Kila Mtanzania Mwenye Ufahamu Wake Anaelewa Nchi Imefika Wapi, Hali Mbaya Kiuchumi Inayoendelea Kuwatesa Wananchi Ndio Kilio Kikubwa Kilichotawala Masikioni Mwetu,

Inasemekana Rais Magufuli Aliwahi Kusema Hakuna Mwanaume Atakaeweza Kubaki Dar Es Salaam Kabla Ya Mwezi Julai Mwaka Huu(Sina Uhakika).

Kwenye Ukurasa Wake Wa Instagram Madee Amepost Video Inayomuonyesha Akiunga Mkono Kauli Hiyo Kwa Maneno Ya Kujigamba...

Wito Wangu Kwenu Wasanii Na Watu Wengine Wenye Ushawishi Muitumie Hii Mitandao Yenu Kuwashawishi Vijana Wa Tanzania Namna Ambavyo Wanaweza Kufanya Vitu Vikubwa Vikaibadili Tanzania Badala Ya Kutumia Mitandao Kujisifia Maisha Yenu Binafsi,

Angalieni wenzenu mbele wanachokifanya wanatumia Muda mwingi Kwenye Mitandao Kuhamasisha Kwa  kuonyesha Maisha Yao Ya Muziki kama studio, Tours Na Vitu kadhaa Vinavyoifanya Career yao kuendelea Kung'aa...
Nafasi Yenu ni kubwa mno Kwenye jamii,

Fanyeni Yale ambayo wabongo watajivunia kuwa Na nyinyi,  hawa mnaoshindwa Kuwahamasisha ndio wale mnaotaka wanunue ngoma zenu, Wawapigie kura mnapokua Nominated Kwenye matuzo Na shows wahudhurie.

Leo msanii wa bongo unamkuta Instagram anavyopiga romance Na baby wake, Na Mifano Mingine Mingi..

https://youtu.be/STyaIR9XALE

No comments