Siku Chache Baada Ya Kusherehekea Siku Yake Ya Kuzaliwa Shetta Ametangaza Hali Ya Hatari


Msanii wa muziki wa bongo fleva, Shetta amefunguka na kuseme siku ya kesho Alhamis amashusha wimbo wake mpya baada ya kimya cha muda mrefu huku akidai kuwa sasa ni wakati sahihi yeye kuachia ngoma hiyo ambayo anasema italeta shida.  

 Shetta akiongea na EATV amesema kesho atakata kiu ya mashabiki wake ambao muda mrefu wamekuwa wakiuliza juu ya ujio wake mpya na kudai kuwa hawezi kuwaangusha kwa kazi hiyo mpya. 

"Kesho naachia mzigo mpya hivyo mashabiki wangu wake mkao mzuri kusikia na kutazama ujio mpya wa Shetta, naamini walini miss sana ila nakata kiu yao kwani huu ni wakati wangu kufanya kweli sasa, wamefanya yao sasa ni zamu ya Shetta kufanya yake" alisisitiza Shetta 
Mbali na hilo Shetta alieleza mahusiano yake na msanii Chid Benz na kusema yeye ameamua kusimama na Chid Benz katika matatizo yake hayo kwa kuwa msanii huyo ni kama kaka yake, hivyo wanagawana umasikini kwa kusaidiana katika mambo mbalimbali.
Theme images by rami_ba. Powered by Blogger.