Sina: Wimbo Mpya Wa Harmonize Ambao Hautaweza Kumuacha Mtu Salama

Baada ya kutuchangamsha na ladha kadhaa zikiwemo Fire, I Miss You na Eneka za Diamond Platnumz, Baadae Sherii Ya Rich Mavoko WCB imetoa mamlaka tena kwa Harmonize baada ya Unaionaje na Young Killer, Kondeboy ameutumia usiku wa Julai 27 kudropisha video ya wimbo wake mpya "Sina".

Kwenye video ameonekana Mfalme wa zamani wa Muziki Afrika Mashariki Mr. Nice aliyejizolea umaarufu katikati ya miaka ya 2000 akitamba na style yake ya TAKEU enzi hizo.

Labda Mr. Nice ametupeleka Behind The Scene ya maisha yake ya nyuma?, Anaonekana ni mtu ambae aliwekeza sana kwenye bata kiasi cha  kusahau hata familia, Baadae mpunga unaisha kila akikatiza mitaa anazomewa mixer kufanya vibarua ili apate ridhiki yake.

Harmonize hashikiki, Kwa ngoma hii amepiga hatua moja mbele, Mdundo safi ulionyongwa na Magic Fingers "Laizer Classic" na Vocal tamu la Harmonize ambalo kwa sikio langu nimehisi kama Harmonize anaanza kuukata U-Diamond, Anyway Enjoy na Hii Video iliyofanywa na Director Khalfan.


 
Mpaka sasa Video hii imetazamwa zaidi ya mara 100,000 ikiwa haijamaliza masaa 24 tayari imo kwenye Top 3 ya zile video zinazo-trend kwenye YouTube ya Tanzania.

No comments