Suti Aliyovaa DJ Khaled Kwenye Kava Ya Grateful Yapigwa Mnada Kisa WanafunziDJ Khaled anatumia nguo zake ili kusaidia wanafunzi kuhitimu masomo yao.

Kwa mujibu wa E! News, Staa huyo wa ngoma "I'm The One" ameungana na Poshmark (Mtandao maarufu kwa uuzaji nguo na mambo ya fashion) kwa ajili ya kuuza nguo zake mwenyewe zitakazoingiza mkwanja wa kuwalipia wanafunzi Ada  na mahitaji yao ya msingi.

Mzigo ulianza kuuzwa tangu jana Julai 12, Kwa kuanza Dj Khaled ameingiza matoleo manne ya kwanza,

Kinachoonekana kuwa kivutio zaidi kwenye ishu hii ni taarifa alizozithibitisha  Dj Khaled kuwa kila nguo itayouzwa haijatengenezwa kwa ajili ya kuuzwa bali ni nguo ambazo miongoni mwao amewahi kuzivaa, 


Miongoni mwa nguo za gharama ambazo DJ Khaled amepanga kuziuza kwenye Campaign hiyo ni suti ya blue ambayo alivaa na mwanae Asahd kwenye kava ya Grateful.