Unyama Ambao Future Ataufanya Kabla Ya Kudondoka Bongo Wikiendi Hii

 Kama ni mfuatiliaji wa mastori ya mastaa wa mbele utakua uliwahi kukutana na picha ambazo Nicki Minaj aliwahi kuzipost miezi kadhaa iliyopita zikimuonyesha sambamba na Rapa Future wakifanya Video ya pamoja.

 Sasa basi kuanzia usiku wa Jumatatu Artwork (Kava) ya ngoma mpya ya Future "You Da Baddest" aliyomshirikisha Nicki Minaj ilianza kusambaa mitandaoni.

Kwenye cover imeonekana mikono ya Rapa hao wakionyesha mikono yao ambayo imejazwa madini ya maana.

 
Future atakua Jijini Dar Wikiendi hii kwenye Show ya Castle Lite Unlocks,
Kwa mara ya kwanza huenda Bongo ikapata chance ya kumuona Future akiperfom ngoma hiyo inayotarajiwa kuachiwa Ijumaa hii.