Video | Kitu Alifanya Aslay Kwenye Stage Ya Maisha Chizika Ndani Ya Maisha Basement
Mashindano ya Pool Table yamefanyika ambapo timu ya Fuoni Pool Club, iliibuka na ushindi na kujinyakulia kombe pamoja na hundi ya shilingi laki tano (500,000) kutoka kwa KIPA, Chama cha Mpira wa Pool Table Wilaya ya Kinondoni, mpango mzima ulikuwa ni ndani ya Ukumbi wa Maisha Basement.

Baada ya zoezi la makabidhiano ya zawadi, ilifuatia shoo ya nguvu kutoka kwa Aslay ambapo kama kawaida yake aliwaamsha vilivyo mashabiki waliokuwa wamefurika kwenye ukumbi huo, wakawa wanaimba naye mwanzo mwisho na kuleta burudani ya aina yake.Nyota ya Aslay ni kama imewaka kwa nguvu kutokana na jinsi mashabiki walivyoonesha kufurahishwa na shoo hiyo mwanzo mwisho na kusababisha shangwe la aina yake ndani ya Ukumbi wa Maisha Basement.

No comments

Theme images by rami_ba. Powered by Blogger.