Calvin Hariss Ndiye DJ Mwenye Mkwanja Mrefu Kawaacha Mbali David Guetta, The Chainsmokers Na Zedd


Moja ya vitu ambavyo huzidi kuliongezea umaarufu Jarida La #Forbes ni kile kitendo cha kutoa takwimu za vitu/Watu ambao hufanya vizuri kwenye nyanja mbalimbali zikiwemo Siasa, Teknolojia, Muziki na mengine mengi.

Kwenye Chapisho la Jarida hilo litakalotoka mwezi Septemba mwaka huu kuna ile Top Ten ya Ma-DJ ambao wameendelea kuvuta mkwanja mrefu kwa kipindi cha mwezi Juni  2016 mpaka Juni 2017.

Albamu yake "Funk Wav Bounces Vol. 1" ambayo imepambwa na majina makubwa yaliyopo kwenye Industry ya Muziki inatajwa kuwa moja ya Chanzo kikubwa cha mapato ya Muingereza Calvin Harris ambae kwa mwaka huu tayari ameshaingiza zaidi ya Dola za kimarekani milioni 48 mkwanja ambao unamfanya kuishika namba moja ya Ma-DJ wanaoingiza mkwanja mrefu kwa mara ya tano sasa.

Ma-DJ Wengine Waliofanikiwa Kutajwa Kwenye Kumi Bora Miongoni Mwa Wanaovuta Mkwanja Mrefu Ni:


1. Calvin Harris ($48.5m)
2. Tiƫsto ($39m)
3. The Chainsmokers ($38m)
4. Skrillex ($30m)
5. Steve Aoki ($29.5m)
6. Diplo ($28.5m)
7. David Guetta ($25m)
8. Marshmello ($21m)
9. Martin Garrix ($19.5m)
10. Zedd ($19m)

No comments