Kwenye Ngoma Moja Wamesimam Saida Karoli, Diamond Platnumz, Darassa, Ben Pol, Belle 9 & GnakoHaukutakiwa kuwa shabiki wake enzi hizo ili kujua ana ngoma kwa wakati huo alipokua akitamba na ngoma zake kama  Mapenzi kizunguzungu (2003) Harusi (2004) Mimi Nakupenda (2005) Nelly (2008) na Chambua kama Karanga (Maria Salome) (2001) ambayo mwishoni mwa mwaka jana tumeona baadhi ya wanamuziki wa bongoflava wakitumia vionjo vyake.

Kabla ya kupotea kwake kwenye Muziki Saida Karoli alikua miongoni mwa wanamuziki waliokua wakimiliki hits nyingi enzi hizo akiwakilisha tamaduni zake za kabila lake la "Kihaya"

Thanks God, Kipaji hakipotei ngoma ambayo ilimpaisha Miaka 15 iliyopita imekua ndio ngoma iliyochangia Mama kurudi kwa kishindo kikubwa, Umeshawahi kufikiria Salome ya Diamond Platnumz na Rayvanny, Muziki Ya Darasa na Benpol Zikiwa zimewekwa pamoja na Give It To Me ya Belle 9 na GNako?, Hicho ndio kitu kinanifanya nakua na mizuka ya kuipa hesima ya #VideoOfTheDay, Idea ya kuchanganya vionjo vilivyotumiwa na vijana waliojaribu ku-copy baadhi ya vitu kwenye ngoma yake mwenyewe vimemfanya Saida Karoli kurudi kwenye ubora wake.

Shoutout kwa Producer Tuddy Thomas kwa kukifanya ambacho waandishi wa ngoma hii walitaka, And big shouout to Hanscana for the stunning Video.

No comments