Taylor Swift - Look What You Made Me Do (Official Music Video)


Alhamisi Agosti 24 mwanamuziki Taylor Swift alitangaza ujio wa Albamu yake mpya "Reputation" Tangazo lililoambatana na Video ya mashairi ya wimbo "Look What You Made Me Do" ambayo ilivunja rekodi ya kuwa "Lyric Video" iliyotazamwa mara nyingi zaidi ndani ya muda mfupi, Mpaka sasa imeshagonga zaidi ya Views Milioni 40.

Video rasmi ya wimbo huo imeachiwa usiku wa jana kwenye utoaji wa Tuzo za VMA inamuonyesha Taylor Swift akifufuka kutoka kwenye kaburi (Zombie), Baada ya muonekano wa kizombi Taylor anabadilika na kuwa kiongozi wa kundi la wanawake maroboti, Jambazi wa Benki na baadae mtu maarufu anaeshambuliwa na kamera za mapaparazi kwenye ajali ya gari.


Kwenye mashairi ya wimbo huu Taylor amekaliliwa akisema "Taylor wa zamani amekufa, aliyepo ni mzimu tu ndani yake.
Zaidi ya masaa 7 ambayo video hiyo imepandishwa kwenye Vevo Channel ya Taylor Swift tayri imeshakusanya zaidi ya views mil 13, Likes milioni 1 na Comment zaidi ya 142,000