Imekua kitu cha kawaida kwa sura au picha za mastaa kuonekana kwenye bidhaa na matangazo mbalimbali either kwa makubaliano au kutokuwepo kwa makubaliano rasmi ya kibiashara, 

Ukifuatilia unaweza kugundua Tupac ni mmoja ya mastaa ambao sura yao imetumika mara nyingi kwenye baadhi ya T-Shirts, Pamoja na kutumia picha ya marehemu Tupac kuuza nguo zao wapo wahusika ambao walikua na makubaliano na timu ya Pac na wengine wamekua wakifanya tu kutokana na kutokuwepo mtu wa kufuatilia umiliki halali wa nembo hizo. Mpiga picha Chi Modu, aliyewahi kufanya kazi na Marehemu Tupac amezishitaki Macy's na Urban Outfitters kwa kutumia moja ya picha aliyowahi kumpiga Tupac. Mpiga picha huyo amedai kuwa Kampuni hizo zilitumia picha hiyo bila idhini yake,

Modu amedai kuwa aliwahi kuingia makubaliano na kampuni ambayo iliuzia kampuni hizo moja ya nembo walizokubaliana, Mkataba wao uliisha tangu mwezi Julai mwaka jana lakini washikaji bado waliendelea kutumia mzigo huo bila kusaini mkataba mwingine, Lengo la mpiga picha huyo kuanzisha kesi ni kutaka kulipwa faida yote iliyopataikana kwa kipindi ambacho kampuni hizo zimekua zikifanyia biashara kazi yake bila kumshirikisha,

Kwa mwaka huu inakua ni kesi ya tatu  kumhusisha 2Pac baada ya ile ya mwanamitindo Kendall Jenner wiki mbili zilizopita kushitakiwa na mpiga picha mwingine wa Tupac kwa kosa hilo hilo la kutumia picha bila idhini kutoka kwa wahusika, Mwezi Juni 2017 mpiga picha Michael Miller aliwashitakia Kendall na mdogo wake Kylie Jenner kwa kutumia picha ya marehemu Pac kwenye moja ya kazi zao,