Mtoto Wa Michael Jackson Anatamani Kuwa Kama Baba Yake Isipokua Kitu Hiki


Prince Jackson ambae ni mtoto wa kwanza wa aliyekuwa mfalme wa muziki wa “Pop” marehemu Michael Jackson amedai hakuwahi kufikiria kama baba yake alikua ni mtu maarufu mpaka alipoziona Video za watu wakizimia kwenye matamasha ya marehemu baba yake.

.
Kwenye mahojiano na The Sun, Prince Jackson ambae alikua ni mtoto mdogo wakati wa kifo cha baba yake mwaka 2009 ameiiweka wazi mipango yake ya kutaka kulienzi jina la baba yake licha ya kutokujua kuimba wala kucheza. 

 “Nimejaribu mara kadhaa mwisho nimegundua Sijui kuimba wala kucheza kama alivyokua Baba yangu, lakini natamani kuienzi nafasi yake kwa namna yeyote ile” Alisema Prince Jackson

“Kitu ambacho nitakiepuka ni kuyaweka maisha yangu binafsi hadharani, Sitoweza kukifanya hicho kitu kwa sababu nataka niwe mtu mkubwa duniani   kama alivyokua baba yangu”
Michael Jackson Enzi Za Uhai Wake Akiwa Na Watoto Wake.
“Nimeanzisha mfuko wa kusaidia watoto wasiojiweza hapa Los Angels ambao unafahamika kwa jina la kumbukumbu ya baba yangu”


Prince Akiwa Na Wadogo Zake Paris na Blanket Kwenye msiba wa Baba yao mwaka 2009
Kwenye kauli nyingine Prince Jackson amesema kwa sasa anafanya kazi ya uandaaji wa Video tena akiwa nyuma ya kamera kuepuka kile alichokisema sio lazima ajiweke waziwazi hata kama anafanya vitu vikubwa na anatamani kuwa na nafasi kubwa kama aliyokua nayo Marehemu Michael Jackson