Ndoa Ya Shilole Na Uchebe Imenukia, Shilole Awaomba Watu Kukaa Mbali Na Mahusiano Yake

Muimbaji wa Bongoflava na staa wa Bongo Movie Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole Kiuno ameiweka wazi siku rasmi ya kufungwa ndoa yake na mpenzi wake wa sasa Ashraf Uchebe.

 Hatua hiyo imekuja baada ya maneno ya kejeli yaliyoandikwa mtandaoni kwenye Instagram Akaunti inayotumika kwa jina la Official_Uchebe (yaani mpenzi wake). 

Shilole amefunguka na kudai kuwa akunti hiyo sio halali kwani mpenzi wake huyo hatumii mitandao.

  "Mpenzi wangu hatumii mitandao, Watu wanataka kutuharibia, Nasemaje wameshindwa maana Disemba 20 ambayo nitakua nikisherehekea siku yangu ya kuzaliwa ndio siku ambayo mimi na mpenzi wangu tutafunga ndoa" AlisemaShilole.

 Angalia Balaa La Shilole Na Adam Mchomvu Hapa, Ni Noma: