Baada Ya Kutangaza Kuuza Magari Rappa Nay Wa Mitego Ametangaza Hili Jipya

Baada ya wiki iliyopita kutangaza kuwa ameuza magari yake yote na kwa sasa anatembelea daladala na bajaji. Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, Nay wa Mitego amekuja na tamasha lake aliloliita ‘Nguvu ya Kitaa’.

Nay wa Mitego amesema lengo la kuanzisha tamasha hilo ni kusaidia mashabiki wake wenye kipato kidogo, kushudia muziki mzuri kutoka kwake na wasanii wengine ambao watamsindikiza kwa bei nafuu.


Tamasha hilo litafanyika mikoa mitano na litajumuisha wasanii kibao wa Bongo Fleva akiwemo QBoy Msafi, Pam D, Chemical na wengineo kibao.

Source: Bongo5No comments

Theme images by rami_ba. Powered by Blogger.